Uhuru anavyopangua hesabu za Ruto na Gachagua 2027 kwa kumnadi Matiang’i

Urejeo wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta katika siasa unaozua tumbo katika kambi ya Rais William Ruto na kuvuruga mikakati ya upinzani. Aliongoza mkutano mkubwa wa Jubilee huko Murang’a akiandamana na Fred Matiang’i, akimtaja kama mgombea urais. Alilia wakazi wa Mlima Kenya wamfuatie ushauri wake kama 2022 na wamge muunge mkono Matiang’i.

Juzi, Bw Kenyatta aliongoza mkutano mkubwa wa hadhara wa chama chake cha Jubilee katika kaunti ya Murang’a akiandamana na mgombea urais wa chama hicho Fred Matiang’i. Jukwaa alilolitumia kurusha mashambulio kwa serikali ya sasa ya Dkt Ruto. Huku akimpigia debe Dkt Matiang’i, rais huyo mstaafu aliwataka wakazi wa Mlima Kenya wamfuatie ushauri wake walivyofanya kuelekea uchaguzi wa 2022 kwa kuupigia kura rais wa sasa.

“Niliwaonya wakati ule lakini hamkusikia na kuamkia kuchagua hawa watu. Si sasa mwajionea?” Bw Kenyatta akasema, bila kutoa ufafanuzi zaidi. Ufasiri wa kauli yake ni kwamba endapo wakazi wangeunga mkono chaguo lake wakati huo, Raila Odinga, hawangekuwa wakilalamika sasa.

Bw Kenyatta alimtaja Dkt Matiang’i kama kiongozi mwenye maono na mchapa kazi anayeweza kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoanzisha wakati wa utawala wake. “Mnamo 2022 niliwaonya kuhusu watu fulani lakini hamkusikia. Sasa nitumai kuwa mko tayari kuunga viongozi ambao wamejitolea kwa dhati kuleta maendeleo nchini Kenya,” akaeleza.

Kauli hiyo imewakera wandani wa Rais Ruto, wanaifasiri kama inayohoji sera za serikali ya Kenya Kwanza. Seneta wa Nandi Samson Cherargei na Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi wameonya Bw Kenyatta dhidi ya kuendelea kuchapa siasa. Cherargei ameonya kwamba endapo ataikosoa serikali, malipo yake yatakatizwa. “Tafadhali Bw Kenyatta kaa nyumbani na utazame jinsi serikali ya Rais Ruto inavyotekeleza sera za kufaidi raia,” akaonya.

Hata hivyo, Profesa Gitile Naituli anasema serikali haiwezi kukatiza haki za Bw Kenyatta za kikatiba. “Nani alimwambia Seneta Cherargei kwamba serikali inaweza kumzuia Bw Kenyatta kufurahia haki zake za kisiasa kwa mujibu wa Kipengele cha 37 cha Katiba,” anaeleza. Hatua ya Bw Kenyatta inakwaza nafasi ya Rigathi Gachagua katika Mlima Kenya kuelekea 2027.

Tovuti hii inatumia vidakuzi

Tunatumia vidakuzi kwa uchambuzi ili kuboresha tovuti yetu. Soma sera ya faragha yetu kwa maelezo zaidi.
Kataa