Mvutano wa Biashara
Mvutano wazuka kati ya kampuni za sukari ukanda wa Magharibi
Mvutano umezuka kati ya kampuni za kusaga miwa eneo la Magharibi baada ya shughuli hiyo kurejea miezi miwili iliyosimamishwa na Bodi ya Sukari nchini (KSB). Kampuni ya Sukari ya Mumias inashutumu Kampuni ya Sukari ya West Kenya kwa uvamizi na wizi wa miwa kabla ya kukomaa. Tukio hili limetokana na ugawaji wa maeneo na madai ya hujuma katika sekta hiyo.