Naibu Rais
Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki amesema hatashawishika na mjadala kuhusu wadhifa wake na anatarajia kuhudumu hadi 2032. Alitoa tamko hili Kaunti ya Meru akijibu Kinara wa ODM Dkt Oburu Oginga ambaye alisema chama chao kinazingatia naibu rais katika mazungumzo na UDA. Kindiki alisisitiza kuwa kiti chake kitasalia na anapanga kusaidia Rais William Ruto kupata kura nyingi kutoka Mlima Kenya.