Mgawanyiko
Mgawanyiko ndani ya chama cha Orange Democratic Movement (ODM) umepanuka baada ya mrengo unaojiita G8 kumshutumu kiongozi wa chama Oburu Oginga kwa hatua zinazochochea migawanyiko. Kundi hilo, linaloongozwa na Waziri Wycliffe Oparanya, limekosoa mrengo wa Oginga kwa kuweka mbele maslahi ya kibinafsi. Viongozi wa G8 wameonya kuunda kundi jingine ikiwa mzozo hautatuliwi.