Marufuku ya Mikaratusi
Mahakama ya Mazingira na Ardhi mjini Ol Kalou imepiga marufuku upanzi wa miti ya mikaratusi ndani ya umbali wa mita 30 kutoka vyanzo vya maji. Jaji Mugo Kamau ameagiza Bunge la Kitaifa kutunga sheria za udhibiti ndani ya miezi 12. Wakati huo, mahakama imetoa maagizo ya muda ya kusimamia upanzi huo.