Mechi Kenya Gambia
Harambee starlets tayari kukabiliana na Gambia kwa kufuzu WAFCON
Harambee Starlets zina dakika 90 leo kukabiliana na Gambia katika mechi ya marudiano ya kufuzu WAFCON 2026. Baada ya kuwashinda 3-1 katika mechi ya kwanza, timu ya Kenya inahitaji kuepuka kufungwa zaidi ya mabao mawili au sare ili kufuzu. Kocha Beldine Odemba amesema timu yake iko tayari kuandika historia baada ya miaka 10 bila mafanikio.