Nyanza
Wanasiasa wanaopigania urithi wa Raila Odinga
Wanasiasa wakuu ndani na nje ya ODM, wengi wao vijana, wameanza mikakati ya siri ya kuwania urithi wa kisiasa wa Raila Odinga baada ya kifo chake. NEC ya chama imemteua Oburu Odinga kama kiongozi wa muda, huku mapambano yakiongezeka katika maeneo ya Nyanza, Magharibi na Pwani. Viongozi kama Gladys Wanga na Babu Owino wamejitokeza kati ya wanaotafuta nafasi hiyo.