Makazi ya mabanda
Zaidi ya familia 100 zimeachwa bila makazi baada ya moto kuzuka usiku wa Jumapili katika eneo la Tulanga, Mukuru Kayaba, Nairobi. Moto ulisambaa kwa kasi kutokana na upepo mkali, na kuharibu nyumba nyingi. Wakazi wamelalamika kwa kucheleweshwa kwa msaada wa dharura.