Treni ya mizigo iliyokuwa ikielekea Mombasa ilishika moto katika eneo la Masimba, kaunti ya Makueni, Jumatano.
Treni ilikuwa ikisafirisha mizigo kutoka Nairobi hadi Mombasa wakati moto ulipozuka kwenye behewa la injini na kuenea hadi behewa tatu au nne za mizigo.
Ripoti zinaonyesha hakuna majeruhi wakati huu, ingawa idadi ya watu walioathirika bado haijathibitishwa. Timu za dharura zilitumwa eneo la tukio ili kudhibiti moto.
Sababu ya moto bado haijafahamika na Kenya Railways haijatoa taarifa yoyote kufikia wakati wa kuchapishwa kwa habari hii. Trenil ilikuwa ikitumia reli ya zamani ya mita.