Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen ametangaza Jumatano Mei 27 kuwa sikukuu ya kitaifa ili kuadhimisha Idd-ul-Adha.
Kupitia notisi ya gazeti iliyochapishwa Jumatatu Mei 25, Murkomen alitangaza kuwa siku hiyo ni ya Idd-ul-Adha ama sikukuu ya kuchinja kwa Waislamu.
“Notified for the general information of the public that, in exercise of the powers conferred by section 3 (1) of the Public Holidays Act, the Cabinet Secretary for Interior and National Administration declares that, Wednesday, the 27th May, 2026, shall be a public holiday to mark Eid-ul-Adha,” ilisema notisi hiyo.
Idd-ul-Adha huadhimishwa siku ya 10 ya Dhul Hijjah baada ya mahujaji kukamilisha ziara ya Hajj huko Mecca, Saudi Arabia. Siku hiyo huamuliwa kutokana na mwaandamo wa mwezi na inaadhimishwa kwa sala, sadaka na kuchinja wanyama.