Afisa wa kaunti aahidi uimarishaji zaidi wa miundomsingi Nairobi

Afisa Mkuu wa Uchukuzi wa Kaunti ya Nairobi Michael Waikenda amesema utawala wa Gavana Johnson Sakaja utaendelea kuimarisha miundomsingi na kuhakikisha usalama wa wanaotembea kwa miguu. Kaunti imewekeza katika ubora wa sehemu za barabara zinazotumiwa na wapitanjia na waendeshaji baiskeli.

Michael Waikenda, Afisa Mkuu wa Uchukuzi wa Kaunti ya Nairobi, alisema utawala wa Gavana Johnson Sakaja utaendelea kuimarisha miundomsingi na kuhakikisha usalama wa wanaotumia njia zilizotengewa wanaotembea kwa miguu. Kaunti imewekeza katika kuhakikisha ubora wa sehemu za barabara zinazotumiwa na wapitanjia, waendeshaji baiskeli na aina nyingine za uchukuzi.

Miradi kama hiyo imetekelezwa katika maeneo ya Westlands, Ngara na katikati mwa jiji, ikichangia kupungua kwa ajali na mizozo kati ya waendeshaji magari na wanaotembea kwa miguu. “Nairobi imekuwa jiji la watu siyo magari pekee. Lengo letu ni kuhakikisha kuna mpangilio bora na uchukuzi unakuwa rahisi sana jijini,” alisema Waikenda wakati akiagua miundomsingi inayoboreshwa.

Sehemu za barabara zinazotumiwa na wapitanjia kwenye barabara za Tom Mboya na karibu na Archives zimechangia kupunguza msongamano wa magari. Aidha, miundomsingi bora imewapa vijana wanaopiga picha ajira na riziki. Maeneo ya Green Park na Desai yameibuka vivutio kwa watengenezaji filamu na abiria kutokana na mandhari mazuri.

Polisi wamekuwa wakitumia teknolojia ya Nairobi Dashboard kukagua na kudhibiti msongamano. “Hii imesaidia kupunguza ajali za barabarani na kuimarisha ushirikiano kati ya polisi wa trafiki,” alisema Waikenda. Kaunti inapanga kushirikiana na sekta za kibinafsi kuimarisha uchukuzi wa mabasi ya umeme, na kubadilisha mienendo ya magari kufuatwa bila utaratibu katikati mwa jiji.

Tovuti hii hutumia kuki

Tunatumia kuki kwa uchambuzi ili kuboresha tovuti yetu. Soma sera yetu ya faragha sera ya faragha kwa maelezo zaidi.
Kataa