Sarah Wairimu amteua wakili Pravin Bowry kumtetea katika kesi ya mauaji

Sarah Wairimu, mjane wa Tob Cohen anayekabiliwa na mashtaka ya kumuua mumewe miaka sita iliyopita, amemteua wakili mwenye uzoefu Pravin Bowry kumtetea. Mahakama imeahihisha kesi hiyo hadi Novemba 27, 2025, huku Sarah akishitakiwa pia kwa kutoa taarifa uwongo kuhusu pasipoti yake. Alinyimwa dhamana na hakimu mkuu Zainab Abdul kutokana na kesi ya mauaji inayoendelea.

Sarah Wairimu, mjane wa Tob Cohen, anayekabiliwa na mashtaka ya kumuua mumewe mnamo Julai 19, 2019, katika makazi yao eneo la Lower Kabete, amemteua wakili Pravin Bowry kumtetea katika kesi hiyo. Mwili wa Cohen ulikutwa umetupwa ndani ya shimo la choo ukiwa umefungwa kwa blanketi. Sarah amekataa shtaka hilo.

Alipofika mbele ya Jaji Diana Kavedza, Bowry aliomba kusoma faili ya kesi na ushahidi kabla ya kusikilizwa. Jaji Kavedza alikubali na akaamuru kesi ihitajwe Novemba 27, 2025, kwa maagizo zaidi.

Wakati huo huo, Sarah alishtakiwa upya mnamo Novemba 7, 2025, mbele ya Hakimu Mkuu Zainab Abdul kwa kutoa habari uwongo kwa Inspekta Mercy Riungu katika kituo cha polisi cha Munyange, Othaya, Kaunti ya Nyeri. Alimdanganya kuwa pasipoti yake nambari BK043532 ilipotea mnamo Februari 20, 2023, na akapata abstrakti ya kupata nyingine. Pia, siku hiyo alimwambia wakili Muchiri WaGathoni uwongo kuwa imepotea na akaapa.

Sarah alikataa mashtaka yote mawili na akaomba dhamana. Upande wa mashtaka ulipinga, ukisema anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji na amenyimwa dhamana na Jaji Kavedza. Hakimu Abdul alitupilia mbali ombi la dhamana, akisema "hastahili kuachiliwa kwa dhamana" kwa kuwa mahakama kuu ilimnyima dhamana mara mbili kutokana na pasipoti mbili na madai ya kutisha mashahidi.

Sarah, kupitia wakili wake wa awali, amekata rufaa dhidi ya kunyimwa dhamana. Abdul alimwambia, "Utasalia ndani hadi mahakama ya rufaa iamue hatma yako ya dhamana. Ikiwa utaachiliwa na mahakama ya rufaa basi utawasilisha upya ombi lako la dhamana." Ameamuru aendelee kuzuiliwa katika gereza la wanawake ya Langata.

Tovuti hii inatumia vidakuzi

Tunatumia vidakuzi kwa uchambuzi ili kuboresha tovuti yetu. Soma sera ya faragha yetu kwa maelezo zaidi.
Kataa