Watu watatu wamefariki baada ya kujaribu kufungua mfereji wa maji machafu katika eneo la Riruta Satellite, Dagoretti, Nairobi.
Mhasiriwa mmoja aitwae Gideon alinaswa baada ya kuingia kwenye mfereji wa maji machafu barabara ya Kabiria ili kuondoa kizuizi kilichoathiri vyoo katika eneo hilo.
Mhasiriwa wa pili, Moses Kithure, mfanyakazi wa ujenzi kutoka kaunti ya Tharaka Nithi, alijiunga ili kutoa msaada lakini pia alinaswa. Mtu wa tatu asiyejulikana alijiunga na juhudi za uokoaji lakini hakutoka.
Wakazi wanasema hakuna hata mmoja aliyetumia kamba za usalama. Miili yao iko katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta, na uchunguzi unaendelea.