Abagusii
Mgombeya urais wa Jubilee, Fred Matiang’i, amefurahia mafanikio ya ziara yake ya siku tatu katika eneo la Gusii, akiandamana na viongozi wa upinzani. Alitumia ziara hiyo kuonyesha ubabe wake katika eneo linalochukuliwa kuwa ngome ya ODM. Pia alipishwa kuwa msemaji wa jamii ya Abagusii na Baraza la Wazee wa Abagusii.