Sekondari Pevu
Maswali mengi yameibuka kuhusu uwezo wa shule za sekondari kuhudumia wanafunzi wapya wanaotarajiwa kujiunga na mfumo mpya wa Sekondari Pevu mwakani. Waziri wa Elimu Julius Ogamba anasema shule zina nafasi ya ziada, lakini wakuu wa shule wengine wana wasiwasi hasa kuhusu miundombinu ya STEM.