Fedha za kaunti
Makubaliano ya siri kati ya magavana na maseneta yamefikiwa na kufifisha mvutano wa wiki kadhaa uliotishia shughuli za kaunti. Magavana wamekubali kushiriki katika vikao vya kamati za Seneti huku maseneta wakiahidi kushughulikia madai ya ufisadi. Mazungumzo makali yalifanyika Senetini na kufikia muafaka.