Nasuri
Mpango wa kutoa matibabu ya nasuri bila malipo uliofanyika Hospitali ya Rufaa ya Murang’a mnamo Aprili 18, 2026, ulisaidia wanawake na wasichana 449. Mpango huo ulileta pamoja serikali ya kaunti, Wizara ya Afya, M-Pesa Foundation, Flying Doctors na Amref Health Africa. Virginiah Wanjira alipata msaada kwa binti yake mwenye umri wa miaka mitano aliye na kasoro ya kuzaliwa inayoitwa congenital ureteric fistula.