GeoPoll
Mahali pa kazi ndilo eneo lenye hatari kubwa zaidi ya unyanyasaji wa kingono barani Afrika, kwa mujibu wa utafiti wa GeoPoll uliofanywa nchini Kenya, Nigeria, Afrika Kusini na Misri. Zaidi ya nusu ya wafanyakazi katika nchi hizo wameripoti kukumbana na hali hiyo, na wanawake wakishika nafasi kubwa. Ripoti inaonyesha asilimia 51 ya washiriki wamepitia unyanyasaji huo kazini.