Ripoti ya Kimataifa
Ripoti mpya inaonyesha kuwa watoto sita kati ya 10 duniani hawajui kusoma sentensi rahisi au kusuluhisha hesabu za kimsingi, ingawa theluthi yao wako shuleni. Hii imezua wasiwasi kuhusu ubora wa elimu katika nchi maskini. Kenya inaongoza majirani zake barani Afrika Mashariki katika vipimo vya hisabati.