Mama Ngina
Mama Ngina Kenyatta na Basil Criticos wamerejea mahakamani wakidai umiliki wa shamba la ekari 2,624 katika Kaunti ya Taita Taveta. Wanadai Msajili Mkuu wa Ardhi amepuuza amri ya mahakama iliyotolewa Desemba mwaka jana. Mahakama imekataa kutoa nafasi ya dharura na kuwapa washtakiwa siku 15 kujibu.