Mvutano chama
Viongozi wa Linda Mwananchi ndani ya ODM wametoa makataa makali dhidi ya mrengo wa Linda Ground ulioongozwa na Seneta Oburu Oginga. Wamesema hawataridhiana hadi maamuzi ya kisiasa baada ya kifo cha Raila Odinga yabatilishwe. Pia wanataka mazungumzo na UDA yasitishwe na ajenda 10 itekelezwe kikamilifu.