Msalaba Mwekundu
Janga la kibinadamu linaendelea kuongezeka Angata Barikoi, Trans Mara, Kaunti ya Narok, baada ya vita vya kijamii vilivyosababisha mauti ya watu nne. Wakimbizi wanaishi shuleni na vituo vya polisi wakikosa mahitaji ya kimsingi. Shirika la Msalaba Mwekundu linaomba misaada kwa familia hizo.