Uongezaji thamani
Viola Maina alijiuzulu kazi katika NMG ili kuanzisha kampuni ya Gooseberry Delight Limited, ambayo inaongeza thamani ya matunda ya zabibubata katika Kaunti ya Uasin Gishu. Alianza kununua matunda hayo kwa bei nafuu na kuyauza, lakini sasa anatengeneza bidhaa kama jamu na juisi. Biashara yake imekua licha ya changamoto za Covid-19.