Wagombea kadhaa wamejitokeza kuwania ugavana wa Kaunti ya Taita Taveta mwaka 2027. Gavana Andrew Mwadime na naibu wake Christine Kilalo wanataka muhula wa pili.
Kaunti ya Taita Taveta haijawahi kuwa na gavana aliyehudumu kwa mihula miwili tangu kuanzishwa kwake. Gavana wa kwanza John Mruttu alishindwa na Granton Samboja mwaka 2017, ambaye naye alishindwa na Andrew Mwadime mwaka 2022.
Bw Samboja ameonyesha nia ya kugombea tena. Wagombea wengine ni pamoja na Mbunge Danson Mwashako, Seneta Jones Mwaruma, Shadrack Mwadime, Anderson Mtalaki na John Mwangemi.
Bw Mruttu sasa anashindania kiti cha useneta. Bw Mwadime aliyeshinda akiwa mgombea huru anaashiria nia ya kutumia chama cha UDA.