Ufugaji kuku
Jogoo mweupe mkubwa ashinda tuzo katika maonyesho ya ASK
Jogoo mweupe wa kilo 5.5 wa aina ya Brahma alikuwa kivutio kikuu katika maonyesho ya kibiashara na kilimo ya Kaunti ya Nairobi 2025, yaliyoandaliwa na Baraza la Kilimo Kenya (ASK). Jogoo huyo, mwenye umri wa miezi tisa, ni mali ya Fredrick Omondi, mfugaji kutoka Kitengela. Ushindi wake ulitokana na ukubwa, afya na utunzaji wake bora.