Gavana wa nairobi johnson sakaja ametangaza kufunguliwa kwa kitengo kipya cha huduma za figo katika hospitali ya mama lucy kibaki.
Kitengo hicho cha kisasa kiko katika hospitali ya level 5 ya mama lucy kibaki katika eneo la umoja ii embakasi magharibi. Kina mashine za kisasa na wahudumu wenye uzoefu ili kutoa huduma za usafishaji damu na matibabu maalumu ya magonjwa ya figo.
Gavana sakaja alisema wakati wa uzinduzi kuwa upanuzi huo utaboresha upatikanaji wa huduma bora na nafuu bila kulazimika kusafiri umbali mrefu. Aliongeza kuwa kitengo kitatoa mipango ya matibabu inayolingana na kila mgonjwa pamoja na ushauri wa lishe na msaada wa nasaha.
Huduma hizo zinapatikana chini ya mpango wa mamlaka ya afya ya jamii. Uzinduzi ni sehemu ya maboresho yanayoendelea katika hospitali hiyo yakiwemo upanuzi wa huduma za wagonjwa mahututi na kumbi za upasuaji.