Rais William Ruto na Seneta Edwin Sifuna wamezua mjadala mkali kuhusu ujenzi wa nyumba za orofa 12 katika eneo la Funyula chini ya Mpango wa Nyumba za Gharama Nafuu.
Mzozo ulianza baada ya Sifuna kuhoji ujenzi huo wakati wa mahojiano katika kituo cha redio cha Mulembe FM Jumatano Julai 22 2026. Alisema nyumba hizo hazilingani na mtindo wa maisha wa jamii za eneo hilo.
Sifuna alitumia mfano wa kufuga kuku akisema "Wamejenga nyumba za orofa 12 za gharama nafuu Funyula. Sisi Waluhya hatuwezi kuishi mahali ambapo kuku wetu hawawezi kuishi. Niambie kuku wako atafikaje kwenye orofa ya 12?"
Rais Ruto alimjibu Alhamisi Julai 23 wakati wa mkutano katika Ikulu ya Nairobi.