Rais William Ruto amesisitiza mpango wa nyumba za bei nafuu baada ya kutia saini Mswada wa Fedha wa mwaka 2026.
Serikali ya Rais Ruto inatarajiwa kutumia karibu Sh220 bilioni katika mpango wa nyumba za bei nafuu kufikia mwisho wa muhula wake wa kwanza mwaka ujao. Zaidi ya nyumba 274,000 zinaendelea kujengwa na mpango huo umechangia kuunda ajira zaidi ya 640,000.
Bajeti ya sekta ya makazi imeongezwa kutoka Sh64.2 bilioni katika miaka mitatu ya mwisho ya utawala wa Uhuru hadi zaidi ya Sh102 bilioni katika miaka mitatu ya kwanza ya utawala wa Ruto. Bajeti hiyo inatarajiwa kufikia Sh138 bilioni katika mwaka wa fedha unaoanza Julai 1.
Rais Ruto alisema mpango huo unasalia kuwa nguzo muhimu ya mageuzi ya uchumi. Hii inatofautiana na urithi wa Rais Uhuru Kenyatta uliojengwa zaidi kwenye miradi ya barabara, reli na kawi.