Mawakili wa Chama cha Gema Watho Association wamedai kuwa kurasa 64 za hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu kutimuliwa kwa Rigathi Gachagua hazipo.
Mawakili hao waliandikia Naibu Msajili wa Kitengo cha Katiba na Haki za Kibinadamu tarehe 12 Juni wakitaka kupata hukumu kamili pamoja na rekodi za kikao cha 8 Juni.
Walisema Jaji Eric Ogola alieleza kuwa hukumu hiyo ilikuwa na kurasa 350 na kwamba majaji watatu waliisoma hadi saa tatu usiku kabla ya kuitia saini.
Nakala waliyopewa siku tatu baadaye ilikuwa na kurasa 286 pekee na haikuwa na saini za majaji. "Ni wazi kuwa kurasa 64 hazipo kwenye hukumu hiyo," walisema mawakili wa Kiragu Wathuta & Company Advocates.