Walimu karibu 40 katika eneo la Pwani wamepata mafunzo ya kukabiliana na itikadi kali kutoka Wizara ya Elimu na NCTC.
Mafunzo hayo yalilenga kuwapa walimu ujuzi wa kutambua mabadiliko ya tabia miongoni mwa wanafunzi mapema.
Mkuu wa Mawasiliano katika NCTC, Bw Charles Opiyo, alisema walimu wana uhusiano wa karibu na wanafunzi hivyo wanaweza kuwasaidia kuepusha dalili za uenezaji itikadi kali shuleni.
Aliongeza kuwa vijana wadogo ndio hulengwa zaidi na makundi ya kigaidi na kwamba mafunzo hayo yanaweza kuokoa maisha.