Naibu Kiongozi wa Chama cha Jubilee Dkt Fred Matiang’i ameonya viongozi wa kisiasa dhidi ya kufadhili makundi ya wahuni na kulaani ghasia zilizosababisha vifo vya watu wasio na hatia.
Dkt Matiang’i alitoa maonyo hayo wakati wa ziara yake katika maeneo ya Keumbu, Gionseri, Bobasi na Nyamokenye katika Kaunti ya Kisii. Alisema serikali ina rasilimali za kutosha kulinda raia lakini imeshindwa kuwazuia wahuni.
Alirejelea shambulio la wiki mbili zilizopita Keumbu ambalo liliua Vincent Osiemo maarufu kama Mapinduzi. Alitangaza kuunda timu ya mawakili na wataalamu wa teknolojia kukusanya ushahidi wa kuwashitaki wahusika na wafadhili wao.
Matiang’i pia alihudhuria mazishi ya Osiemo Gionseri na kumpongeza Rigathi Gachagua pamoja na chama cha DCP kwa ushindi wa uchaguzi mdogo wa Ol Kalou. Alisisitiza umoja wa Wakenya kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.