Brian Kiprop Kipglagat alikamatwa mpakani mwa Namanga Juni 10, 2026, na sasa anazuiliwa rumande Nairobi akisubiri uamuzi wa kurudishwa London kujibu mashtaka ya kumuua mpenziwe Maryanne Nduta Januari 2025.
Mahakama ya Milimani ilimsikiliza Kiplagat Juni 12, 2026, mbele ya Hakimu Mwandamizi Daisy Mutai. Mkurugenzi wa mashtaka Bi Joyce Olajo aliiambia mahakama kuwa mshukiwa huyo anatarajiwa kushtakiwa chini ya sheria za mauaji za Uingereza, ambazo zinafanana na zile za Kenya.
Kiplagat alikamatwa alipojaribu kuingia Tanzania. Polisi wa Uingereza walikuwa wametoa hati ya kumtia nguvuni kupitia Interpol na Huduma ya Kitaifa ya Polisi.
Mahakama iliamuru mshukiwa huyo abaki chini ya ulinzi wa Polisi wa Kupambana na Ugaidi hadi Juni 15, 2026, ili kuruhusu kukamilika kwa utaratibu wa kumsafirisha kwenda Uingereza.