Kiongozi wa ODM Dkt Oburu Odinga amemkosoa Gavana wa Siaya James Orengo kwa kuzingatia siasa za kitaifa badala ya kutatua matatizo ya wenyeji.
Akizungumza Siaya, Dkt Oburu alisema Orengo anapaswa kushughulikia barabara mbovu, ukosefu wa maji, huduma duni za afya na kucheleweshwa kwa mishahara ya wafanyakazi wa kaunti.
Alimhimiza gavana kushirikiana na serikali ya kitaifa ili kupata miradi zaidi, badala ya kushiriki maandamano dhidi ya serikali.
Dkt Oburu alipongeza wanachama wa ODM kwa kutoshiriki maandamano ya Gen Z ya hivi karibuni na akasema chama hakina haraka ya kuingia mazungumzo ya miungano kabla ya uchaguzi wa 2027.