Ibada ya kuwaaga wanafunzi 15 waliokufa kwenye moto wa bweni la Shule ya Upili ya Utumishi Girls Academy, Gilgil, ilijaa machozi na majonzi.
Moto ulioteketeza bweni la shule hiyo ulisababisha vifo vya wanafunzi hao.
Viongozi waliohudhuria walijumuisha Gavana wa Nakuru Susan Kihika, Maseneta Tabitha Karanja na Edwin Sifuna, Mke wa Rais Rachel Ruto, na Waziri wa Elimu Julius Ogamba.
Hali ya kukata tamaa ilitawala wakati wa ibada hiyo iliyofanyika Kaunti ya Nakuru.