Viongozi wa ODM kutoka Kaunti ya Homa Bay wameahidi kuungana ili kumpatia Rais William Ruto kura eneo hilo.
Waziri wa Fedha John Mbadi aliongoza wito wa umoja huo Jumapili katika kanisa la Kiadventista la Sombro, Kochia, eneobunge la Rangwe.
Viongozi walioshikana mikono ni pamoja na Gavana Gladys Wanga, Katibu Raymond Omollo, Waziri Opiyo Wandayi, Mbunge Joyce Osogo na Seneta Moses Kajwang’.
Wao waliahidi kuhakikisha Rais Ruto anapata kura zote za eneo la Nyanza mwaka 2027 huku wakisisitiza kuwa marehemu Raila Odinga aliwaacha ndani ya Serikali Jumuishi.