Chama cha UDA kinachoongozwa na Rais William Ruto kinatumia miradi ya maendeleo kuvutia wapigakura katika uchaguzi mdogo wa eneobunge la Ol Kalou utakaofanyika Julai 16.
Maafisa wa ngazi ya juu serikalini wamekuwa wakizindua miradi mbalimbali katika eneo hilo. Waziri wa Ardhi Alice Wahome na Waziri wa Utalii Rebecca Miano ni miongoni mwa viongozi waliozuru Ol Kalou.
Wikendi iliyopita Wahome aliwaongoza maafisa wengine kufungua afisi ya ardhi Nyandarua na kutoa vyeti 2700 vya ardhi. Wahome alisema hatua hiyo ni ya kihistoria kwani inahamisha huduma karibu na wananchi.
Mnamo Juni 2 Miano alifungua kituo cha reli cha Ol Kalou. Mbunge wa Gatanga Edward Muriu amekosoa hatua hiyo akisema miradi haitawashawishi wapigakura.