Rais William Ruto alimaliza ziara yake ya siku nne Luo Nyanza ikiwa na miradi mingi ya maendeleo. Ziara hiyo iliyojaa miradi inasemekana imesambaratisha juhudi za upinzani na Linda Mwananchi kupata uungwaji mkono eneo hilo kuelekea 2027. Mchanganuzi anaonya kuwa ikikamilika miradi hayo kabla ya uchaguzi, upinzani utakuwa shakani.
Rais William Ruto alitamatisha ziara yake ya siku nne Luo Nyanza Jumapili, akiwa na miradi ya mabilioni katika kaunti kama Vihiga, Kakamega, Busia na Bungoma. Mnamo Jumamosi, Ruto na Rais Yoweri Museveni wa Uganda walizindua ujenzi wa reli ya kilomita 107 kutoka Kisumu hadi Malaba, ikikamilisha reli ya kilomita 1000 kutoka Mombasa-Malaba na kuunganisha na Kampala.