Mabadiliko ya tabianchi yameathiri uzalishaji wa chakula nchini Kenya, na wataalamu wanashauri wakulima kugeukia mazao yanayohimili ukame.
Dkt Ndungu Kabare kutoka Ruiru amesema mazao kama mtama, wimbi, teff, amaranth na chia yanahitaji maji kidogo na hukomaa haraka. Yanatoa mavuno mawili kwa mwaka tofauti na mahindi.
Mazao haya yana thamani ya lishe ya juu ikiwemo madini, vitamini na antioxidants. Pia yana kiwango cha chini cha sukari kinachoingia haraka mwilini hivyo yanafaa kwa wagonjwa wa kisukari.
Soko la mazao haya linaendelea kukua kutokana na mahitaji ya vyakula bora kiafya. Viwanda vya kusaga nafaka na chakula cha mifugo vinahitaji malighafi hii.
Kupanda mazao haya kutapunguza utegemezi wa mahindi na kuimarisha usalama wa chakula nchini Kenya, alisema Dkt Kabare.