Chama cha Uanahabari katika Shule ya Upili ya Kairi Boys, Gatundu Kaskazini, Kaunti ya Kiambu, kinaendelea kuwakuza wanafunzi katika fani za lugha na mawasiliano.
Wanachama hukutana baada ya masomo ili kujadili mikakati ya kuendeleza chama. Wanafunzi hushiriki katika shughuli zinazohusiana na ualimu, tafsiri, upigaji picha na uhariri.
Chama kinatarajia kuanzisha kitengo cha uigizaji na kuzindua jarida rasmi la shule mwaka ujao. Wanafunzi wanaoshiriki wameonyesha mafanikio katika mitihani ya Kiswahili na Kiingereza pamoja na kujiamini zaidi.
Mlezi Bi Doreen Kathurima alisema chama hicho kinaboresha matokeo ya KCSE na maendeleo katika ulumbi na utangazaji. Mwalimu Mkuu Bw Anthony Mwaria alisema kinawaandaa wanafunzi kwa taaluma za uanahabari.